Jumanne 30 Desemba 2025 - 21:30
Wananchi wa Italia wafanya maandamano makubwa kwa ajili ya kuiunga mkono Palestina

Hawza/ Italia katika siku mbili zilizopita ilishuhudia migomo mikubwa ya kitaifa kwa wingi, pamoja na maandamano makubwa katika miji yake mikuu. Maandamano haya yalifanyika kwa lengo la kuonesha mshikamano na watu wa Ghaza na pia kudhihirisha hasira dhidi ya sera za ndani na za nje za Italia.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, mgomo wa saa 24 wa vyama kadhaa vikubwa vya wafanyakazi nchini Italia uliathiri na kuvuruga sekta muhimu, zikiwemo usafiri wa umma, reli, anga (ndege), huduma za serikali na elimu. Vyama vya wafanyakazi vinasema kuwa sera za kiuchumi na kijamii za serikali ya Italia zinaweka mzigo usio wa haki juu ya familia zenye kipato cha chini na wafanyakazi, jambo linalosababisha hali kubwa ya kukata tamaa miongoni mwa wananchi.

Hata hivyo, migomo ya siku zilizopita ilizidi kwa haraka malalamiko ya kiuchumi na kijamii, na ikachukua sura ya kisiasa na kibinadamu yenye nguvu zaidi. Safari hii, katika miji mbalimbali ya nchi hiyo, maelfu ya wafanyakazi, wanafunzi na wanaharakati wa haki za binadamu waliandamana chini ya bendera ya Palestina, wakitaka kusitishwa kwa vita vya Ghaza, kutozingirwa, na kuungwa mkono raia wa Ghaza na Ukingo wa Magharibi.

Waandaaji wa maandamano haya walisema kuwa; vita hivi na mauaji ya halaiki “vimefanya mazungumzo kuhusu heshima ya binadamu au haki za kijamii kuwa jambo lisilowezekana, ilhali watoto na wanawake wanauawa kila siku huko Ghaza.”

Maandamano na migomo hii ni uhamasishaji wa pili mkubwa wa vyama vya wafanyakazi vya Italia katika wiki za hivi karibuni katika kuiunga mkono Palestina, hali inayoonesha wazi wimbi linaloongezeka la uungwaji mkono wa umma kwa haki za Wapalestina, pamoja na kuongezeka kutoridhika barani Ulaya kuhusu vita vinavyoendelea.

Chanzo: EUPAC

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha